MKOA WA KATAVI KUPATIWA MADAKTARI BINGWA



Na.Issack Gerald
Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa itakayopatiwa madaktari bingwa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wangonjwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu waziri wizara ya Afya Dk Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa viti maalumu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA Roda Kunchela aliyetaka kujua lini serikali italimaliza tatizo hilo.
Akijibu swali hilo amesema tayari serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kulikabili suala hilo kwa mkoa wa Katavi na maeneo mengine.
Licha ya hayo serikali ya mkoa wa Katavi iko mbioni kuanza ujenzi wa hosipitali ya rufaaa itakayo toa huduma kwa mkoa mzima ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 1 ilikwishapatikana kwa ajili kuanza ujenzi wa Hospitali hiyo.
Mwezi Julai mwaka huu,Waziri wa afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia ,wazee na watoto mh.Ummy Mwalimu aliahidi kuleta pesa mkoani Katavi ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Katavi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA