NDEGE IMEANGUKA ARUSHA NA KUUA WATU 11
Shirika
la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali ya
ndege iliyotokea jana asubuhi limesema watu wote 11 waliokuwa katika
ndege hiyo wamefariki dunia.

Shirika
hilo limesema majina ya waliofariki katika ajali hiyo bado hayajawekwa wazi
wakisubiria kuwajulisha ndugu zao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Coastal,Julian Edmunds amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana,
na kwamba mara kadhaa amekuwa akisafiri na ndege za shirikia hilo na hivyo anaimani
na marubani pamoja na ndege zao.
Aidha,ameeleza
kuwa kwa niaba ya shirikia hilo na wafanyakazi wake, watafanya kila
litakalowezekana ndani ya uwezo wao kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo
kwani hakuna kitu cha umuhimu kwao zaidi ya usalama wa abiria.
Kwa
sasa wameeleza kwamba wanafanya uchunguzi katika eneo la tukio na kuwa, taarifa
zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa kamili
zitakapopatikana.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments