ZAIDI KAYA 40 ZINALALA NJE MKOANI KATAVI

Issack Gerald-Mpanda Katavi
Zaidi ya kaya 40 katika manispaa ya Mpanda  hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na upepo uliosababishwa na mvua zinazoendelea  kunyesha.

Wakazi wa maeneo ya Kazima ringini,Kilimani na Kaparangao ambao wamekumbwa na adha hiyo jana na wamesema nyumba zao zimeharibiwa kabisa na kwamba sasa wanalazimika kulala nje.
Aidha wananchi hao wamesema licha ya viongozi mbalimbali kufika katika maeneo hayo yaliyokumbwa na majanga akiwemo mkuu wa wilaya na viongozi wengine hakuna msaada wowote walioupata.
Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa wa Kazima Ringini Dionisi Clement amesema serikali lazima ichukue hatua za haraka kuwasaidia wananchi hao.
Mwaka uliopita maafa kama hayo yalitokea maeneo mbalimbali mkoani Katavi.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA