DC TANGANYIKA: HATUKUJUA KAMA WANANCHI WANA SILAHA ZA KUPAMBANA NA ASKARI



MKUU wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando,amesema mwananchi aliyepigwa risasi na askari na kufariki dunia akiwa katika Hospitali ya Wilaya Mpanda,alipigwa risasi wakati wa majibizano ya risasi kati ya wananchi na askari.

Mkuu wa Wilaya akizungumza na Mpanda Radio amesema majibizano kati ya askari na wananchi hao wa eneo la Mnyamasi linalodaiwa kuwa ni sehemu ya msitu wa hifadhi lililotekea Jumamaosi Oktoba 7 mwaka huu.
Licha ya kuwa mtu aliyefariki alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda, Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dkt.Theopista Elisa jana amesema hawezi kusema ikiwa aliyefariki pamoja na wengine wane walilazwa katika Hosiptali hiyo wanatokana na sakat hilo.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyamasi Bw.Magosha Mtoveka amesema tukio hilo ambalo lilianza juzi na kuendelea mpaka jana pamoja na askari hao wa maliasili kupiga ovyo risasi za moto pia vyakula na mali nyingine inaelezwa zimechomewa ndani ya nyumba zao.
Awali imedaiwa askari walifika kijijini hapo na kuanza kuwafurusha wakazi wa eneo hilo kwa kutumia nguvu na silaha za moto kwa madai kuwa wamevamia hifadhi ya msitu wa Mnyamasi ambapo watu saba wanatajwa kurehiwaa.
Suala hilo linaleta hali ya wasiwasi kwa kuwa Mtu yeyote aliyejeruhiwa ili apatiwe matibabu lazima majeruhi apatiwe fomu namba tatu (PF3) kutoka polisi inayoeleza tukio lililompata ambapo watu wanahoji iweje mpaka jana Mganga ashindwe kubainisha chanzo kilichopelekea watu hao kufikishwa kutibiwa katika hospitali hiyo.
Kwa mjibu wa sheria za Tanzania Askari haruhusiwi kutumia risasi za moto kumpiga mwananchi ambapo matukio mengine kama hayo ya watu kupoteza maisha yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA