RC KATAVI : WAZAZI MKOANI KATAVI WANAOKATISHA MASOMO WATOTO WAO KUKIONA CHA MOTO

Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa mkoa wa Katavi Meja jenerali mstaafu Raphael Mugoya Muhuga,amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheri dhidi ya wazazi wanawakatisha masomo wanafunzi kwa tamaa ya kujipatia mahali.

Muhuga ametoa kauli hiyo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo kimkoa yameadhimishwa katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema ripoti ya vifo vya uzazi vinavyotokea Mkoani Katavi inaonyesha hutokana na   mimba   katika  umri mdogo  kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 18.
Kwa upande wa  Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Mpanda Agness Buraganya pamoja na mambo mengine amewataka wazazi na walezi kuachana na  tamaduni za kizamani kwa kuona kuwa mtoto wa mwenzie haifai kumkanya anapokosea masuala kadhaa.
Wakati wa kongamano la siku hiyo lililofanyika jana Mjini Mpanda likishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,ripoti katika mkoa wa Katavi inaonesha katika kipindi cha 2012-2016 wanafunzi wapatao 258 walikatizwa Masomo kwa sababu ya mimba.
Hata hivyo huenda takwimu hizo zikawa zimeongezeka mpaka kufikia mwaka huu kwa kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu,mimba kadhaa za wanafunzi zimeripotiwa katika Halmashauri za Mkoa wa Katavi ikiwemo Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo yenye wanafunzi 14 waliopatwa na mimba katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Siku ya mtoto wa kike duniani iliasisiwa na umoja wa mataifa  Desemba 2011 lengo likiwa kutafuta shida na dhuluma kwa mtoto wa kike katika mataifa mbalimbali.
Katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yameadhimishwa Wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo “Kauli mbiu inasema tokomeza mimba za utotoni kufikia uchumi wa viwanda

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blohspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA