CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI KATAVI CHAFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI WILAYANI TANGANYIKA



Na.Issack Gerald-Katavi
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoani Katavi,kimefuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Bw.Yasin Mohamed Kibiriti kuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Tanganyika.

Katibu wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Kajoro Peter Vyohoroka pamoja na mambo mengine amesema kamati ya Halmashauri kuuya CCM mkoani Katavi imeamua kufuta matokeo ya uchaguzi wa ccm wilayani Tanganyika katika nafasi ya Mwenyekiti,Katibu wa siasa na uenezi na wajumbe wote wa kamati ya siasa ya Halmashauri kuu.
Amesema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kutokana na mwenyekiti anayetakiwa kushindwa kupata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa huku mwenyekiti aliyekuwa akidaiwa kushinda akitangzwa kinyume na kanuni za chama hicho.
Wakati huo huo Msimamizi mkuu Bw.Chrisant Mwanawima amepatiwa adhabu kwa mjibu wa kanuni na maadili ya chama kwa kushindwa kwake kusimamia uchaguzi huo huku akijua kuwa anavunja kanuni ya uchaguzi kwa kuwa wakati anatangaza matokeo hakumshirikisha msaidizi wa uchaguzi ambapo ilionekana ilikuwa ni kumpendelea Bw.Yasin Kibiriti.
Kwa mjibu wa matokeo yaliyotangazwa Yasin Mohamed Kibiriti alipata kura 222,Abdallah Salum Sumry kura 175,Mombo Rashid Mombo kura 53 ambapo jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 458,kura halali 450 huku kura 8 zikiharibika.
Kikao maalumu cha kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Katavi chini ya mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Mselem Abdallah Said kilikutana Juzi Oktoba 9,baada ya kupokea malalamiko juu ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 6 mwaka huu.
Kwa mjibu wa Katibu wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Kajoro Peter Vyohoroka msimamizi wa uchaguzi hakuzingatia kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2012 ibara ya 11(b) na Ibara ya 21(b).
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA