WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI KESHO KUPATIWA ELIMU YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Na.Issack Gerald-Katavi
IDARA ya maendeleo ya ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kesho inatarajia kuendesha semina kwa watu wenye ulemavu ili kuwapatia elimu ya namna ya kujikwamua na umaskini kwa kufanya shughuli za maendeleo.

Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoani Katavi Bw.Issack Lucas Mlela amethibitisha hatua hiyo ya Halmashauri kuleta semina hiyo kwao na kusema semina hiyo itakuwa mwanga kwao kufanya shughuli za maendeleo zenye tija.
Mwezi uliopita,Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi lilisikika likilalamika kusahaulika kwa watu wenye ulemavu katika fursa za maendeleo hususani katika ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali kutoka idara za maendeleo ya jamii.
Mkoa Wa katavi unakadriwa kuwa na watu wenye ulemavu zaidi ya 2000 huku wakigawanyika katika makundi ya watu wasioona,wenye usonji,ulemavu wa ngozi albino,ulemavu wa viungo,kutosikia(viziwi) na wenye mtindio wa ubongo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA