SEKTA YA UCHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI,VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

Vijana mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa ya machimbo ya madini ya dhahabu yaliyopo mkoani Katavi katika kujiinua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wanaofanya shughuli hiyo katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Dirifu Mjini Mpanda.
Katika hatua nyingine wachimbaji hao wamewataka vijana kupuuza maneno ya baadhi ya watu kuhusiana na kazi ya uchimbaji madini kwani migodini kuna shughuli mbalimbali ambazo hazihatarishi maisha ya wachimbaji.
Licha ya sehemu nyingi za wachimbaji wadogo wadogo kutokuwa rasmi, uchimbaji wa madini ni moja kati ya sekta iliyoajiri vijana wengi mkoani Katavi 
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA