RPC KATAVI:WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HAIKUBALIKI

Na.Issack Gerald-Katavi
Kamanda wa polisi Mkoa wa katavi Damasi Nyanda ametoa wito kwa wananchi katika halimashauri ya wilaya ya Mlele kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati wanapowakamata.

Kamanda Nyanda ametoa wito huo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kalovya kata ya Inyonga ambapo amesema suala la wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kumuua kwa kumchoma moto mtuhumiwa haikubaliki bali watuhumiwa wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Amesema zaidi ya watu wapatao 77 wameuawa wilayani Mlele kwa kipindi cha mwaka 2015 huku mpaka kufikia mwaka huu kwa mjibu wa kamanda Nyanda watu wapatao 150 wameuawa kutokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Kwa upande wa makosa ya ubakaji,kamanda Nyanda amesema mpaka mwezi Juni mwaka huu makosa 46 ya ubakaji yameripotiwa katika jeshi la polisi huku visa vya watu kujinyonga,kukutwa wamekufa navyo vikionekana kuwa katika hali ya juu.
Katika kipindi cha Oktoba 7 mpaka Oktoba 14 mwaka huu watu 6 wameripotiwa kuuwawa ambapo matukio yote yameripotiwa kutokea Wilayani Tanganyika baadhi yakihusisha kuigwa na vitu vizito na watu wasiojulikana huku wengine wakipigwa risasi.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA