MANISPAA YA MPANDA YATOA ELIMU KWA WATU WENYE ULEMAVU

Na.Issack Gerald-Katavi
HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imeendesha semina kwa watu wenye ulemavu,ili kuwaelekeza njia sahihi wanazotakiwa kutumia ili kukidhi vigezo vya kupewa mikopo kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo.

Katika semina hiyo,Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Mpanda Linus Kalindo,amewataka watu wenye ulemavu Manispaa ya Mpanda kuainisha shughuli wanazoweza kuzifanya kwa ufasaha ili mikopo watakayopewa iwe chachu ya maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA)Mkoani Katavi Issack Mlela,amewataka watu wenye ulemavu kupuuza maneno yanayowakatisha tamaa kuwa watu wenye ulemavu hawawezi kufanya shughuli za maendeleo.
Makundi ya watu wenye ulemavu ambayo yameshiriki katika semina hiyo ambayo imefanyikia shule ya msingi Azimio, imewashirikisha watu wenye ulemavu wa kutoona,kutosikia, viungo na wenye ulemavu wa ngozi aulibino.
Julius Kipeta,Prasida Kameme na Godfrey Sadara Pamoja na mamb mengine wametaka haki zao za msingi hasa mambo yanayogusa suala uchumi zizingatiwe ili kutoendelea katika lindi la umaskini.
Afisa maendeleo ya Jamii Manispaa ya Mpanda Bw.Linus Kalindo kusema kuwa kuna mifutko mitatu ya vijana,wanawake ambayo ni ya kitaifa pia amesema kuna mfuko wa wajasiliamali katika wilaya ya Mpanda.
Wakati huo huo ameahidi  kufuatilia katika bajeti ya Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda ili kujua kiasi cha fedha walichotengewa watu wenye ulemavu kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuwa hata mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu alisema katika mgawanyo wa asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmshauri,vijana hupata 4%,wanawake 4% na watu wenye ulemavu 2%.
Kikao kingine kitakachowaelimisha watu wenye ulemavu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuunda vikundi kinatarajiwa kufanyika wiki ijayo kikishirikisha watalaamu wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda na makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la Jamhuri ya Muunano wa Tanzania mwaka 2010,inaitaka serikali na jamii,kutoa haki sawa katika kila Nyanja kama elimu,afya na huduma nyingine za kibinadamu.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA