WALIMU WAKUU MKOANI TABORA WALALAMIKIA UFINYU BAJETI YA RUZUKU YA ELIMU BURE-Oktoba 5,2017



Na.Issack Gerald
WAKUU wa shule wamelalamikia kutotosheleza kwa kiwango cha fedha ambacho kimekua kikitolewa na serikali kuu kwamba hakikidhi mahitaji na wameiomba serikali kuongeza kiwango cha fedha  ambazo zimekua zikitolewa kama ruzuku kwa ajili ya kusaidia wanafunzi mashuleni.

Hayo yamebainishwa katika mkutano ambao umewakutanisha wadau mbalimbali wa elimu katika ukumbi wa chuo cha veta mjini Tabora kupokea mrejesho wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za ruzuku kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Mkutano huo umeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali ya Haki elimu kwa kushirikiana na mtandao wa marafiki wa Elimu Mkoani Tabora.
Miongoni mwa mambo ambayo yamejadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na  suala la sera ya elimu bure huku baadhi ya walimu wakitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuongezea fedha za ruzuku kwa ajili ya kuendesha maendeleo ya shule kwa kuwa fedha ambayo imekuwa ikitolewa na serikali kuu inakuwa haijitoshelezi.
Kwa upande wake Imani Mwakalinga ambaye ni mwenyekiti wa mtandao wa elimu Mkoani Tabora amesema kuwa bado kuna changamoto ya matumizi ya fedha hizo ambapo wananchi kwa kiasi kikubwa hakuna uwazi wa taarifa za mapato na matumizi kwa kuwa hata ushirikishwaji wa wananchi umekuwa mdogo kwani hakuna fedha zinazochangwa na wananchi kwa kiwango kikubwa.
Naye mbunge wa jimbo la Tabora Mjini Emmanuel Mwakasaka amesema bado wananchi wana nafasi ya kushirikishwa katika michango ambayo siyo mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya shule.
Aidha zaidi ya Shilingi Milioni 236 zimekuwa zikitolewa na serikali kwa ajili ya uendeshaji wa sera ya elimu bila malipo kwa shule za msingi 76 na shule za sekondari zipatazo 23 zilizopo Mkoani Tabora.
huku wananchi.
Mwandishi:Amisa Mussa,Mhariri-Issack Gerald
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA