JESHI LA POLISI MKOANI RUKWA WATAJA MAJINA YA WALIOKUFA KATIKA AJALI-Oktoba 5,2017



Na.Issack Gerald-Sumbawanga
JESHI la polisi mkoani Rukwa limetoa majina ya watu 15 waliofariki katika ajali ya Fuso lenye namba za usajili T425 BFF ili ndugu zao wakachukue miili ya marehemu kwaajili ya kwenda kufanya maziko.
Kamanda wa polisi mkoani humo Georege  Kyando alisema kuwa miili ya watu waliokufa katikaajali hiyo  ni wanawake 10 nawanaume watano huku baadhi ya ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Nkasi. 
Aliwataja marehemu hao kuwa ni Domona Tenganamba(41),Emaanuel Rashif(84),Restuta Sunga(35) Salula Revena(38)FeresiaTenganamba(12)
Prisca Madeni(45).
Aliwataja wengine kuwa ni mwalimu washuleya msingi Kalambanzite,  Richard Chikwangara(24)Yusta Somambuto(36),Giles Ramadhani(24),
Odetha Madirisha(46)Megi Nalunguli(52)
Kamanda Kyando Aliwataja wengine kuwa ni Abuu Amani Mandevu(37)Nyandindi Batrahamu(35) Magdalena Mbalamwezi(50) pamoja na mtoto mwenye umri wa wiki mbili ambaye bado hajapewa Jina.
Pia aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Dismas Clement(26),Sema Savery(25)Ally Haruna(33),Yusta Mfundimwa(50)Tenesfory Oscar(36) Amos Kitambale(25) Neema Mwanandenje(21)Joseph Sungula(28) namwanamke mmoja ambaye Yupo chumba cha wagonjwa mahututi I. C. U na hajafahamika jina lake mpaka sasa. 
Alisema kuwa marehemu na majeruhi wa ajari hiyo ni watu kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini ni vizuri wananchi wakafuatilia ili kujua kama kuna ndugu yao wafanye mawasiliano kwani serikali iliahidi kusafirisha maiti mpaka watakapofanya maziko.
Alisema kuwa dereva wa gari hilo bado anasakwa na atakapopatikana afikishwe mbele ya sheria kwa uzembe nakusababisha ajali iliyo sababisha vifo hivyo. 
Naye mkuu wa wilaya  ya Nkasi Said Mtanda alimshukuru rais John Magufuli kwa kuungana na wafiwa wote katika katika kipindi hiki cha majonzi kwa kuondokewa na ndugu zao kwa ajali mbaya ya gari. 
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA