CWT KATAVI WAICHARUKIA SERIKALI SUALA LA STAHIKI ZAO-Oktoba 5,2017



Na.Issack Geral-Katavi
CHAMA cha walimu Tanzania CWT mkoani Katavi,kimeitaka serikali kulipa madeni pamoja na malimbikizo mbalimbali ya walimu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha walimu Tanzania CWT Mkoa wa Katavi Hamisi Ismaili ikiwa leo ni siku ya walimu Duniani.
Amesema serikali imekwishafanya uhakiki wa Madeni hayo ya walimu hivyo kama imeridhishwa ni vema kulipa kwani walimu wameanza kukata tamaa.
Wakati huo huo baadhi ya walimu kutoka shule mbalimbali za Manispaa ya Mpanda,wamesema kukosekana kwa mazingira rafiki ya kazi ni kikwazo katika kuwaandaa wanafunzi watakaoleta tija kwa taifa.
Madai haya yanajiri ikiwa ni siku chache tu tangu Rais wa Tanzania DK John Pombe Magufuli kusema hana mpango wa kuongeza mishahara.
Tamko hilo la Rais limwaacha wengi wa watumishi wa umma wakishangaa kauli ya rais inayoleta mkanganyiko tofauti na kauli aliyokuwa ameitoa awali mei mosi siku ya wafanyakazi duniani kuwa kuanzia mwezi julai katika mwaka wa fedha 2017/2018,serikali italipa mishara kwa wakati,itaongeza mishahara kwa watumishi wa umma,kupandisha madaraja na kulipa malimbikizo ya madeni yote inayodaiwa serikali.
Hata hivyo shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limesema limeshtushwa na tamko la rais John Magufuli na ambapo wamesema wanatarajia kukutana ili kujadili tamko hilo ikiwa ni pamoja na kuketi kiti kimoja na serikali kwa ajili ya maslahi ya watumishi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA