KAMATA KAMATA WASIOKUWA NA VYOO MKOANI MBEYA-Oktoba 5,2017



Na.Issack Gerald
WANANCHI wa Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wanakabiliwa na ukosefu wa vyoo bora.

Katika kukabiliana na hali hiyo,Halmashauri imeanza kuchukua hatua za kuwafikisha Mahakamani wananchi wasiokuwa na vyoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Busokero Eston Ngilangwa amesema Kampeni ya usafi itakuwa endelevu huku akisema kuwa amepata upinzani kutoka kwa wananchi kuhusu suala la usafi huku akisema hata lifumbia macho.
Aidha amesikitishwa na baadhi ya wanasiasa wanaopinga hatua anazochukua dhidi ya wananchi wasiokuwa na vyoo wakisema kuwa watakosa kura kipindi cha uchaguzi.
Hata hivyo amesema hatasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayekwamisha suala la vyoo na atachukua hatua bila kujali cheo au wadhifa alionao.
Halmashauri ya Busokero inashika nafasi ya 182 kwa kusafi kati ya Halmashauri 185 zilizopo nchini ambapo Halmashauri hiyo ina historia ya kukumbwa na ugonjwa kipindupindu mwaka 2016.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA