DC MLELE AFUNGUA MAFUNZO YA UANDAAJI BAJETI KISASA-Oktoba,5,2017



Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
MKUU wa Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Recho Kasanda,leo amefungua mafunzo ya siku tano ya uandaaji bora wa bajeti unaojulikana kama PLANEP kwa wakuu wa idara katika Halmashauri hiyo pamoja na wafanyakazi waandamizi ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mlele.

Katika mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Inyonga,Kasanda amesema mfumo huo utaongeza uwazi,uwajibikaji pamoja na kupunguza gharama za serikali katika halamshauri hiyo.
Mfumo huo wa bajeti kwa njia ya kielektroniki unatarajiwa kutumika kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019.
Mafunzo hayo yaliyoanza Jumatatu ya wiki hii yatahitimishwa kesho.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA