WAPENZI WA JINSIA MOJA WAKAMATWA ZANZIBAR-Septemba 16,2017

Mamlaka ya kisiwani Zanzibar imewakamata watu 20 wanaotuhumiwa kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mjibu wa Afisa mkuu wa Polisi Zanzibar Hassan Ali,Wanawake 12 na wanaume 8 walikamatwa kufuatia uvamizi wa polisi katika hoteli moja ambapo washukiwa hao walikuwa wakishiriki katika warsha.
Mapenzi ya jinsia moja ni uhalifu nchini Tanzania na ngono miongoni mwa wanaume ni hatia inayomtia hatiani mhusika na kufungwa kifungo cha kati ya miaka thelathini jela na kifungo cha maisha.
Mwezi Septemba mwaka 2016,serikali ilisitisha kwa muda miradi ya ukimwi ya wapenzi wa jinsia moja ambap pia mwezi Februari mwaka huu,serikali ilisitisha huduma za vituo 40 vya afya vya kibinafsi kwa madai ya kutoa huduma kwa wapenzi wa jinsia moja.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA