UNDENI VIKUNDI FEDHA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEAMAVU ZIPO-Septemba 16,2017

SIKU moja baada ya Shirikisho la watu wenye Ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi kuomba watu wenye ulemavu kuwezeshwa ili kujikwamua kimaisha na hatimaye kujenga uchumi wa taifa,halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imewataka watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya kijasiliamali ili wapatiwe mikopo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu kuhusu haki ya watu wenye ulemavu katika kupatiwa mikopo ili kufanya shughuli za maendeleo.
Bw.Nzyungu amesema fedha ipo isipokuwa wanachosubiri ni vikundi vya watu wenye ulemavu kujitokeza ili kupatiwa mikopo hiyo yenye masharti nafuu.
Aidha amesema mpaka sasa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Manispaa ya Mpanda imetoa Shilingi milioni thelathin (30,000,000/=) kwa vikundi vya wajasiliamali ambapo watu wenye ulemavu hawamo katika kiasi hicho kutokana na kutokuwa na vikundi.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya asilimia 10 zinazotolewa kwa vikundi vya wajasiliamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Katika mgawanyo wa asilimia 10 kwa makundi hayo ambapo ni sawa na shilingi milioni 200,wanawake hupata asilimia 4 vijana asailimia 4 huku watu wenye ulemavu wakipata asilimia  2 ambapo kwa kiasi kikubwa wanawake wameonekana kujitokeza kupata mikopo hiyo kwa wingi ukilinganisha na vijana wanaojitokeza kwa uchahche huku kukiwa hakuna watu wenye uleamavu wanaojitokeza.
Siku ya jana Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi kupitia kwa mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw.Issack Lucas Mlela liliomba serikali iwapatie mikopo watu wenye ulemavu ili kujikwamua kimaisha.
Makundi ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi yanahusisha walemavu wasioona,walemavu wa viungo,viziwi,walemavu wa akili,walemavu wenye tatizo la usonji na wenye ulemavu wa ngozi Albino ambapo jumla ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi wanakadiriwa kuwa zaidi ya 1000 wakiwemo wanafunzi karibu 100 wanaosoma katika shule za msingi Kashato,Nyerere na Azimio zenye vitengo maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2010 ,serikali pamoja na jamii kwa ujumla inawajibika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki sawa na wale wasio na ulemavu katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Uchumi, Biashara na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya binadamu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA