MLIPUKO WA KIPINDUPINDU MBEYAWATU 8 WAFARIKI DUNIA 628 WAPATIKANA NA UGONJWA HUO-Septemba 16,2017

DC Wilayani Mbarali Reuben Mfune
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Mh.Reuben Mfune ameagiza bar zote,migahawa,vilabu vya pombe na grocery kufungwa kwa siku zisizojulikana kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kuzidi kusambaa wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ametoa taarifa hiyo kupitia Afisa habari wa wilaya hiyo Daudi Nyingo na kuwataka wananchi kuwa makini na matumizi ya maji ya mito na mifereji kwa kuwa yameathiriwa na vijidudu vya kipindupindu.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mbarali amesema mtu yoyote ambaye atakiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria

Hadi kufia Septemba jana,wagonjwa mia sita na ishirini na nane wamepatikana huku jumla ya watu nane wakifariki dunia kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA