SHIVYAWATA WAOMBA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZESHWE ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI-Septemba 15,2017

SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi,limesema watu wenye ulemavu mkoani Katavi bado wanahitaji kuwezeshwa zaidi kama makundi mengine yasiyo na ulemavu ili kujikwamua kimaisha na kujenga uchumi wa taifa.

Mwenyekiti wa shirikisho hilo Mkoani Katavi Bw.Issack Lucas Mlela amesema,makundi ya watu wenye ulemavu yameendelea kuishi katika maisha magumu kutokana na kutopewa kipaumbele kama sheria ya nchi inavyoelekeza.
Aidha Bw.Mlela ameyapongeza mashiriki binafsi ambayo yamekuwa yakitoa semina kwa watu wenye ulemavu ili kutambua haki yao na wajibu wa jamii kuhusu makundi hayo.
Makundi ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi yanahusisha walemavu wasioona,walemavu wa viungo,viziwi,walemavu wa akili,walemavu wenye tatizo la usonji na wenye ulemavu wa ngozi Albino ambapo jumla ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi wanakadiriwa kuwa zaidi ya 1000 wakiwemo wanafunzi karibu 100 wanaosoma katika shule za msingi Kashato,Nyerere na Azimio zenye vitengo maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2010 iliyopitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2010 ,serikali pamoja na jamii kwa ujumla inawajibika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki sawa na wale wasio na ulemavu katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Uchumi, Biashara na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya binadamu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA