NDOA ZA JINSIA MOJA ZAMFIKISHA MAHAKAMANI-Septemba 16,2017

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu Mkazi wa Manispaa ya Mtwara, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa.

Akisoma kesi hiyo hakimu mkuu mkazi Richard Kabate amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kabate amedai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi na mwezi wa Juni mwaka huu akiwa katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara kwa makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.
Hata hivyo hakimu Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba.
Mara baada ya Mshtakiwa kusomewa  shtaka hilo na wakili wa serikali George Makasi amekana shitaka hilo na upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.
Mshtakiwa amerudishwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 28 mwaka huu ambapo dhamana iko wazi baada ya mwezi mmoja.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA