SITA WAFA MAJI BAADA YA GARI KUSOMBWA NA MAJI KATAVI, ZAIDI YA WATANO BADO KUPATIKANA,MKUU WA MKOA APIGA MARUFUKU MAGARI KUSAFIRI KUPITA MTO KOGA


Na.Issack Gerald-Katavi
Watu wapatao 6 wameripotiwa kupoteza maisha katika daraja la mto Koga lililopo mpakani mwa mikoa ya Katavi na Tabora, baada ya maji yaliyotokana na mvua kufurika na kusababisha watu hao kusombwa na maji.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari alisema watu hao waliosombwa na maji baadhi ya miili 6 hadi sasa haijaonekana ambapo kati ya hao ni wanawake wawili na watoto wanne.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa watu hao wamefikwa na umauti baada ya gari aina ya Toyota Pick Up yenye namba za usajili T597 BTC, kusombwa na maji wakati likijaribu kuvuka Mto Koga.
Kufurika maji kwa daraja la Mto Koga, kumesababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya miji ya Mpanda mkoani Katavi na Sikonge mkoani Tabora, na kusababisha kero kubwa kwa mamia ya abiria.
Miongoni mwa waathirika hao ni wanawake na watoto, wanaotumia miundombinu kwa ajili ya kwenda kliniki na shuleni, wamelazimika kulala eneo la mto huo kusubiri maji yapungue.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, ajali hiyo ilitokea juzi saa 12 jioni baada ya gari hilo lililokuwa likitokea Tabora kwenda mjini Mpanda kufika katika eneo hilo la Mto Koga na kukuta foleni ya magari yakisubiri kuvuka.
Inadaiwa kuanzia juzi zaidi ya magari 100 yalikuwa yamekwama huku idadi kubwa ya abiria wakikwama pia katika eneo hilo na kulazimika hadi maji yapungue.
Hata hivyo majina ya walikufa katika ajli hiyo hayajafahamika.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Mussa Juma ambaye ndiye aliyekwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Inyonga  amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni.
Katika gari hilo lililozama lilikuwa na watu 11 ambapo kati ya hao watano wamethibitishwa kufariki dunia huku Dreva wa gari hilo akiokolewa.
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ndiye Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk. Ibrahimu Msengi ametoa agizo kwa viongozi wa usalama Mkoani Katavi kusitisha safari za mabasi,gari ndogo na gari za mizigo  kutoka Mpanda-Tabora na Tabora-Mpanda kutokana na daraja la mto koga kukatika na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watano.
Endelea kuwa na P5 TANZANIA MEDIA kujua zaidi idadi kamili ya waliofariki kutoka jeshi la polisi

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA