MKUU WA WILAYA NKASI ATOA RAI KWA MADIWANI WILAYANI HUMO KUHAKIKISHA WANATATUA CHANGAMOTO YA MAPATO YA HALMASHAURI


Na.Issack Gerald-Nkasi.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Idd Hassan Kimanta amewaasa madiwani wa Wilaya hiyo kuhakikisha suala la kukuza mapato ya Halmashauri inakuwa ajenda ya kudumu kwao.

Akizungumza kwenye kaikao cha baraza la madiwani Mkuu huyo wa Wilaya amesema madiwani wengi wakati wakiwasilisha taarifa zao za kwenye kata, kila mmoja ameeleza changamoto kadhaa zilizopo kwenye kata yake na kutaka zitatuliwe na Halmashauri.
Bw.Kimanta amesema suala la kukuza mapato halitawezekana  kama halmashauri haitakuwa na fedha za kutatua changamoto hizo.
Halikadhalika Kimanta amewataka madiwani kushirikiana na wataalam wa Halmashauri ili kupata suluhisho la kukuza mapato ya ndani ya Halmashauri na kuweza kutoa huduma sahihi kwa wananchi wanaowawakilisha.
Katika Wilaya ya Nkasi wamekuwa wakikumbwa na changamoto za kukosa masoko ya mazao,matatizo ya kukosa miundombinu bora ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa,nyumba za walimu na changamoto nyingine za kimaisha.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA