ASKARI POLISI KATAVI APIGWA RISASI YA TUMBONI AFA PAPOHAPO ENEO LA TUKIO- P5 TANZANIA INAKULETEA UNDANI ZAIDI


Na.Issack Gerald-Mpanda
Askari wa jeshi la polisi Mkoani Katavi H305PC Nobert Stanslaus Chacha amekufa baada ya kupigwa risasi maeneo ya Kapanda juu kata ya Machimboni Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa askari huyu amekufa baada ya kupigwa risasi ya tumboni na risasi kutokea mgongoni.
Tukio hilo limetokea baada ya mkazi wa Kapanda kuvamiwa na watu wasiojulikana ambapo baada ya mkazi huyo kufayatua risasi ndipo ikampata askari huyo.
Kamanda amesema kuwa Mwili wa Marehemu Chacha umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA