TANZANIA YATANGAZA MIKAKATI ZAIDI UJENZI MIUNDOMBINU YA BARABARA KATAVI


Na.Issack Gerald-Dodoma
Serikali imesema kuwa inaendelea na mikakati ya kuhakikisha inatenga fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi barabara za Mkoa wa Katavi kwa kiwango cha lami kuunganisha na maeneo mengine jirani kwa ajili ya kukuza uchumi mkoani Katavi.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Tanzania bungeni Mjini Dodoma Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda vijijini Mheshimiwa Suleiman Kakoso aliyetaka kujua mipango ya serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara Mkoani Katavi.
Juzi Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kuwa mwaka huu wa 2016 baadhi ya barabara Mkoani Katavi zikiwemo zinazounganisha mkoa wa Rukwa na Katavi zitakuwa zimekamilika.
Naibu waziri Ngonyani alisema ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Mpanda umegawanyika katika sehemu nne, ambazo ni Sumbawanga kanazi kilometa 75, Kanazi-Kibaoni Kilometa 76. 6, Kibaoni- Stalike kilometa 72 na Stalike-Mpanda kilometa 36.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA