TAARIFA KAMILI YA POLISI KUHUSU WATU KUFA MAJI KATAVI BAADA YA GARI KUSOMBWA NA MAJI HII HAPA,POLISI WASUBIRI MIILI IELEE NDIPO IOKOLEWE


Na.Issack Gerald- Katavi
Miili mitano ya watu walikufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji katika Mto Koga uliopo mpakani mwa Mkoa wa Katavi na Tabora imepatikana huku miili mingine mitano ikiwa hajajulikana ilipo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa hadi sasa wanasubiri miili hiyo mitano ambayo haijapatikana mpaka itakapoibuka na kuelea ndipo juhudi za uokozi zifanyike.
Katika tukio hilo,miongoni mwa ambao hawajapatikana ni pamoja mama mmoja ambaye alikuwa na watoto wanne.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa tukio hilo linahusisha gari aina ya Toyota Pick Up yenye namba za usajili T597 BTC.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Mussa Juma ambaye ndiye aliyekwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Inyonga  wakati wakisaidia kuvusha gari hilo kabla ya kusombwa na maji amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni.
Hata hivyo Bw.Mussa amesema kuwa mambo yanayotakiwa kufanyika katika eneo hilo ni ujenzi wa mnara wa mawasiliano,ujenzi wa kituo cha polisi,uwekaji wa alama katika daraja hilo ambalo limekatika kabisa na kujenga daraja ambalo maji hayawezi kupita juu yake kama ilivyo sasa.
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ndiye Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk. Ibrahimu Msengi ametoa agizo kwa viongozi wa usalama Mkoani Katavi kusitisha safari za mabasi,gari ndogo na gari za mizigo  kutoka Mpanda-Tabora na Tabora-Mpanda kutokana na daraja la mto koga kukatika na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watano.
Hili linakuwa tukio lingine la kusikitisha katika historia ya Mkoani Katavi baada ya Basi la kampuni ya Sumry High Class likiwa mtoni baada ya kupata ajali saa 7:30 usiku kuamkia Julai 5, 2013 katika Mto Iku katika kijiji cha Sitalike wilayani Mlele mkoani Katavi ambapo maiti tisa ziliopolewa katika ajali hiyo na majeruhi 53.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA