BIL.31 ZAPITISHWA NA BALAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA MWAKA WA FEDHA 2016/2017


Na.Lutakilwa Lutobeka-Mpanda
Jumla ya madiwani 20 katika halimashauri ya wilaya ya Mpanda wamepitisha bajeti ya shilingi bilioni 31 ya mwaka 2016/2017 iliyopendekezwa na halmashauri hiyo.

Hayo yamejiri baada ya kikao cha kujadili bajeti ya halmashauri ambapo Afisa mipango wa halmashauri hiyo Bw. Phosphors Nsuri amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia dira ya maendeleo ya halmashauri ikiwa pamoja na huduma za kijamii na miundombinu.
Aidha pamoja na kupitisha bajeti hiyo madiwani wameiomba halmashauri kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao ili kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mheshimiwa Hamad Mapengo amewataka madiwani kuwajibika ipasavyo katika kata zao kwa kusimamia miradi iliyopo katika kata hizo.
Mbali na kikao hicho cha balaza la madiwani kuhudhuriwa madiwani hao, pia kikao hicho kimehudhuriwa na watalaamu mbalimbali kutoka katika halmashauri ya wilaya ya  mpanda pamoja na wanasiasa mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA