WANAFUNZI WANYESHEWA MVUA WAKISOMEA CHINI YA MIEMBE WILAYANI MPANDA,WAZAZI WAISHIWA NGUVU WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA


Na.Issack Gerald-Mpanda
Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Sambwe iliyopo mtaa wa Kampuni  Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,wameiomba serikali kuwasaidia kumalizia ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ili wanafunzi hao waondokane na adhaa ya kunyeshewa na mvua  inayoambatana na radi wakiwa chini ya miembe.
                                                        
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Sambwe wanavyoonekana katika picha katika madarsa yaliyokuwa yakitumika mwezi septemba mwaka jana ambao hata hivyo miti hiyo unayoiona hakuna mti hata mmoja wanasomea chini ya mwembe
                                             
Moja ya mwembe unaotumiwa na wanafunzi kama darasa ukitumika kama ukumbi wa mikutano ya wazazi Shule ya msingi Sambwe

Hayo yamebainishwa na wazazi hao wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda Radio Katika mtaa huo,kuhusu namna wazazi wanavyojitolea katika ujenzi wa madarasa shuleni hapo.
Aidha wamesema kuwa,baadhi ya watoto wamekuwa wakiugua magonjwa kama homa,maralia na mengineyo huku daftari zikilowana kutokana na wanafunzi kukosa mahala pa kujisitiri.
Baadhi ya Wazazi waliozungumza ni pamoja na Mussa Daudi,Huruma Washega na Peter Paul Masesela wote wakazi wa Mtaa wa Kmpuni ambao pia wamesema kutokana na kuishiwa pesa hawana namna zaidi ya kuitegemea serikali kutokana na uwezo wao kufikia kikomo.
Hata hivyo wameeleza kusikitishwa na serikali kuwafukuza wachimbaji wadogowadogo katika mgodi wa Kampuni ambapo wachimbaji hao kila mara wamekuwa sehemu mojawapo ya chanzo cha Mapato katika kuendesha maendeleo ya shule.
Katika hatua nyingine,wameiomba serikali kumuweka  katika mfumo wa malipo mwalimu Alex Sangu ambaye amekuwa akifundisha katika shule ya Sambwe kwa muda mrefu ikizingatiwa kuwa hawana tena uwezo wa kulipa kutokana na kipato chao kidogo kinachotosheleza kuendesha familia zao.
Hata hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw.Charles Kassian ,hakuwa tayari kuzungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio kuhusu maendeleo na hali ya shule zaidi ya kusema kuwa labda atazungumza baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Kampuni Bw.James Simon amekiri wanafunzi kusomea chini ya miembe tangu shule zifunguliwe  Januari 11 mwaka huu ukizingatia kuwa ni msimu wa mvua za masika zinazoambatana na radi.
Hata hivyo Bw.Simoni,amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati masuala mbalimbali yakiwemo kumlipa mwalimu wakati yakifanyiwa kazi ambapo wakati huo huo amesema kuwa siku ya jumatano ya wiki ijayo wanatarajia kuitisha mkutano wa hadhara kujadili maendeleo ya shule.
Shule ya Msingi Sambwe,ina walimu 2 walioajiriwa na seriklai huku mmoja akiwa ni wa kujitolea ambo shule hiyo iliyosajiriwa mwaka huu ina wanafunzi wapatao 150 kuanzia darasa la kwanza hadi la nne.
Hata hivyo Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw. Philipo Mbogo ambaye ni miongoni mwa walioanzisha shule hiyo baada ya kuona kuwa watoto wanahangaika kwenda kusomea umbali mrefu,ameiambia P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Radio Kuwa suala la shule hii linafahamika na linafanyiwa kazi.
Siku ya jana,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alitoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi kujikinga na mvua sehemu iliyo salama ikiwa ni pamoja na kueupa kwenda chini ya miti ambapokwa kiasi wanafunzi hawa  hawatofauriani na mazingira kama hayo kwa kuwa hakuna madarasa.
Mshirikishe na mwezio Kuhusu P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA