MAAFISA ELIMU NSIMBO WAPEWA SIKU 6 KUHAKIKISHA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA SEKONDARI WANARIPOTI


Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
MAAFISA elimu sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo wamepewa siku 6 kuanzia jana, kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanaripoti.

Akizungumza juzi katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele kanali mstaafu Issa Suleiman Njiku, amesema mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza si mazuri na kuwataka maafisa elimu kushirikiana na wenyeviti na watendaji wa vitongoji, vijiji na kata, kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti shuleni.
Aidha Kanali Njiku ameutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kuhakikisha unatekeleza tamko la Waziri wa TAMISEMI juu ya kutatua changamoto ya upungufu wa madawati.
Amesema mkoa wa Katavi umetoa muda  hadi mwisho wa mwezi Machi, kuhakikisha halmashauri zote zinatekeleza agizo hilo, na halmashauri ambayo haitatekeza, Mkurugenzi atachukuliwa hatua za kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA