WANANCHI KATAVI WATAKA VIONGOZI WA SERIKALI WAMUENZI SOKOINE KWA KUPELEKA HUDUMA MUHIMU ZA JAMII KWA WANANCHI


Wananchi Mkoani Katavi wamewashauri viongozi wa serikali wa serikali ya awamu ya tano kuenzi kifo cha Wazairi Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine kwa kupeleka huduma muhimu za kijamii kwa wananchi ikiwemo maji.
Wakizungumza na P5TANZANIA kwa nyakati tofauti kuhusu kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha waziri mkuu hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki Apriki 12,1984 wamesema kuna maeneo mengi mkoani Katavi ambayo bado yanakosa huduma muhimu kama maji huku hata sehemu zenye zikipata kwa mgao.
IAidha wametaka hata miradi ya maji iliyoanzishwa enzi za ukoloni ifufuliwe huku wakisema bado kuna hali ngumu ya kimaisha ambayo serikali inatakiwa iyatatue kama sehemu ya kumuenzi Sokoine.
Aidha wamesema ni kiongozi aliyechukia uhujumu uchumi,rushwa,ufisadi huku akishiriki vema kuandaa majeshi wakatio wa vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda mwaka 1978.
Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili Februaei 13 mwaka 1977 hadi Novemba 7 mwaka 1980 na  Februari 24 mwaka 1983 hadi kifo chake kwa ajali ya gari Mkoani Morogoro akitokea Bungeni Dodoma kuelekea Jijini Dar es salaam.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA