RAIS MAGUFULI ATAKA WATANZANIA WAMUEZI SOKOINE KWA KUIGA MEMA ALIYOYAFANYA


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli ametoa rai kwa watanzania kumuenzi Waziri Mkuu wa Zamani hayati Edward Moringe Sokoine kwa kujenga umoja,kupiga vita rushwa na kuchapa kazi.
Rais ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia Aprili 12,1984 kwa ajali ya gari.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Dakawa nje Kidogo ya Mji wa Morogoro wakati akitokea Bumgeni Dodoma Kuelekea Jijini Dar es salaam.
Amesema watanzania wanapoazimisha siku hii ya kifo chake, watanzania waige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa,mpiga vita rushwa,ufisadi,unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa.
Rais amesema kwa upande wake anamkumbuka kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa la Tanzania na anasema alipata taarifa za kifo cha Sokoine  tarehe 12 Aprili 1984 akiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi katika kikosi cha “Oparesheni Nguvukazi”.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA