LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 34 YA KIFO EDWARD SOKOINE HISTORIA YAKE IKO HAPA

Edward Moringe Sokoine (1938 - 12 Aprili 1984) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania.
Aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili,tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980,tena tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake,alipofariki kufuatana na ajali ya gari.
Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
Upande wa dini,alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki,tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
Sokoine alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa ilipangwa.
Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.
Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli,mkoani Arusha.
Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha Sokoine"ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA