SPIKA AAGIZA MWANDISHI NA WAHARIRI WA GAZETI LA RAIA MWEMA WAHOJIWE KWA KULIDHALILISHA BUNGE


Kamati ya Maadili,Haki na Madaraka ya Bunge,inatarajia kuwahoji mwanahabari Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti la kila wiki la Raia Mwema kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha bunge,Aprili 9 wiki hii.
Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge,Job Ndugai aliyesema kuwa habari iliyochapishwa Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge.
Hayo yamekuja baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?”haidhalilishi bunge.
Spika Ndugai leo Aprili 12,ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA