RAIS AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo Aprili 12,2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali.
Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo,Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.
Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.
Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali.
Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1 kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.
Waliopandishwa vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu,J.J Mwaseba, A.S Mwamy,R.K Kapinda,C.D Katenga,Z.S Kiwenge,M.A Mgambo,A.M Alphonce,A.P Mutta,A.V Chakila,M.G Mhagama,V.M Kisiri,C.E Msolla na S.M Mzee.
Wengine ni C.J Ndiege,I.M Mhona,R.C Ng’umbi,S.J Mnkande, A.C Sibuti,M.M Mumanga,I.S Ismail,M.N Mkeremy,G.S Mhidze,M.A Machanga,S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E Gaguti.
Halikadhalika Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Luteni Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Kanali na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais (Aide de Camp – ADC)
Kanali Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka Naziad Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA