WANANDOA WAFA MAJI



Watu wawili ambao ni wanaondoa wamefariki dunia katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuchukuliwa na mafuriko katika mto Piyaya Kata ya Piyaya wilayani humo.
Picha hii haina uhusiano wowote na habari hii ni kuonesha picha maji tu
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amesema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji ya mto huo wa msimu kupungua.

Aidha,Kamanda Ilembo amewataja marehemu hao kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto wa mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.
Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA