RAIS MAGUFULI AAGIZA WAFANYABIASHARA WADOGO WA STENDI MOROGORO WASIBUGHUDHIWE


Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina  moja la Avintishi,leo amejitoa kimasomaso na kumueleza Rais John Magufuli kuhusu kero wanayopata wafanyabiashara ndogondogo ikiwamo kunyang’anywa bidhaa zao.
Mwanamke huyo ametoa kero hiyo leo,katika uzinduzi wa kiwanda cha Sigara cha Philip Morris mkoani Morogoro.
Baada ya kueleza hayo,Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro,John Mugarula kujibu kero zilizoibuliwa na mama huyo ambapo Mkurugenzi huyo, alisema wanawaondoa wafanyabiashara hao kwa sababu wametengewa maeneo maalumu huku akisema sababu ya suala la kipindupindu.
Baada ya hapo Rais,alimuhoji mama huyo,ni kiasi gani alitozwa na askari mgambo wa manispaa,mama huyo akaeleza kuwa alitozwa Shilingi 200, 000.
Rais alihoji tena,iwapo mama huyo anamkumbuka askari mgambo aliyemtoza kiasi hicho? Ambapo Baada ya kusema hayo,Rais alimpa mama huyo fedha na kumtaka mkurugenzi kumpa kiasi kingine cha fedha mama huyo.
Kufuatia hatua hiyo,Rais aliagiza kuanzia leo,wafanyabiashara hao wasibughudhiwe kwa sababu ni watoto wa maskini.
Wageni wengine waliokuwapo katika uzinduzi huo ni Mbunge wa Viti Maalumu,(CCM) Getrude Rwakatare ambaye ni miongoni mwa waliomchangia mwanamke huyo fedha.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA