MWANAFUNZI AFARIKI MAZINGIRA YA KUTATANISHA POLISI WAWASHA TAA NYEKUNDU



Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato cha sita Sundi George.
Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Juma Bwire amesema mwanafunz huyo alikuwa akisoma katika shule ya sekondari Mwembetogwa.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Kamanda Bwire amesema mnamo Machi 12 mwaka huu mwanafunzi huyo akiwa na sare za shule alitoka nyumbani kwao kuelekea shuleni lakini hakurudi hadi mwili wake ulipopatikana  maeneo hayo.
Kamanda Bwire amesema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo.
Hata hiyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa mtu yoyote anayehusika katika tukio hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA