MAKAMU WA RAIS AFUNGIWA MAISHA

Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Michael Wambura amefungiwa kifungo cha maisha cha kutojihusisha na mchezo wa soka popote pale.
Michael Wambura
Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kuwa Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF.
Ndimbo alisema  Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo,kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi ambapo Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea.
Alisema kamati hiyo iliyokaa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wake Hamidu Ally Mbwezereni,wamemkuta na makosa matatu yatakayomfanya Wambura asijihusishe na masuala ya soka.
Kosa la kwanza amevunja kifungu no 73 kwa kupokea malipo yasiyo halali ya TFF, ambapo faini yake ni milioni 10, kutojihusisha na soka miaka mitano au maisha.
Kosa la pili kugushi malipo kwa jina la TFF enzi hizo (FAT), ambapo amezuiliwa kujihusisha na soka kwa miaka 5.
Kosa la tatu linalomkabili ni kushusha hadhi ya TFF,kosa ambalo adhabu yake iliyotolewa ni kutojihusisha na soka maisha.
Kwa upande mwingine,Kamati ya Maadili ya TFF imesema adhabu hiyo iliyotolewa dhidi ya Michael Wambura imezingatia vigezo na masharti.

Hata hivyo,wakili wake Emmanuel Muga amesema,hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14, 2018).
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA