ACT-WAZALENDO WALAANI UHARIFU MKOANI KATAVI


Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoani Katavi, wamelaani matukio mbalimbali ya uharifu yanayoendelea kujitokeza Mkoani Katavi na kusababisha mauaji ya raia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo John Malack pamoja na katibu wa chama hicho Bw.Joseph Mona wamevishauri vyombo vyote vya ulinzi na usalama kutafuta namna ya kudhibiti waharifu ili kuimarisha usalama wa raia ma mali zao.
Kwa upande wao baadhi ya vijana Mkoani Katavi wamesema, ukosefu wa ajira kwa vijana wengi waliopo mitaani ni miongoni mwa vyanzo vinavyochangia kuongezeka kwa uharifu.
Kuanzia mwezi Januari mpaka Machi mwaka huu,zaidi ya watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti yakiwemo matukio mawili ya ujambazi Januari 27 kata ya Ugalla,Februari 25 mwaka huu katika Mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo wilayani Mpanda na lingine la Januari 22 likihusisha kifo cha mwanafunzi aliyeuwawa kikatiri wilayani Tanganyika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA