RAIS MAGUFULI ASEMA ANAPATA TABU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Pombe Magufuli amekiri kupata
wakati mgumu katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri kutokana na kuwa Mkoa wa
Singida kujaa Wabunge wenye sifa zote za kushika nyadhifa hizo.

Rais amesema kwamba Wabunge
wa mkoa huo wamekuwa wakimfurahisha katika utendaji kazi wao wa kuwatumikia
wananchi.
Aidha
Rais Magufuli amekiri kufurahishwa na wakazi wa Singida kwani wamekuwa
wakitekeleza kauli ya 'Hapa Kazi Tu' kwa vitendo kwa kulima sehemu kubwa
ya mkoa huo ambapo amejionea mwenyewe akiwa katika safari ya gari kuelekea
mkoani hapo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments