BARAZA LA WAKUNGA LATOA TAMKO
Baraza
la Uuguzi na Ukunga Tanzania limelaani na kutoa pole kwa Wauguzi kutokana na
matukio yaliyofanywa na viongozi ikiwemo kuwekwa rumande na kupigwa katika
mazingira yao ya kazi.

Matukio hayo ya
udhalilishaji yanajumuisha tukio lililotokea Machi 7 mwaka huu katika Hospitali
ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Muuguzi Amina Luena Nicodemus aliwekwa ndani kwa
amri ya Mkuu wa Wilaya kwa tuhuma za kuuza nguo za watoto akiwa kazini.
Tukio
lingine lililotokea tarehe Machi 8 mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu ambapo Muuguzi Hilda Ebunka alipigwa na Diwani akiwa kazini akitoa huduma.
Viongozi
wa kitaifa,ikiwa ni pamoja na Mhe.Waziri Mkuu,Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi
ya Rais TAMISEMI na Mheshimiwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto kwa nyakati mbalimbali wamekemea na kusisitiza mamlaka mbalimbali
kuepuka kufanya vitendo vya udhalilishaji wa Wauguzi na Wakunga.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments