WILAYA YA MPANDA KUANZISHA KILIMO ZAO LA PAMBA NA KOROSHO-Oktoba 6,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Pamba
MKUU wa wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga, amesema Wilaya ya Mpanda imetenga Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kuanzisha kilimo cha zao la pamba kuanzia mwaka huu 2017.
Korosho

Matinga amebainisha hatua hiyo wakati akizungumza kuhusu uanzishwaji wa mazao mbadala ya kibiashara Mkoani Katavi.
Amesema jumla ya hekta 1236 zinatarajiwa kulimwa katika msimu wa kilimo mwaka 2017/2018 ambapo mpaka sasa wakulima wapatao 639 wamejiandikisha kuanza kulima zao hilo huku matarajio ikiwa ni kuvuna tani mbili hadi tatu.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 wakulima wapatao 68 walilima zao hilo na kuvuna tani 35 zilizouzwa wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambapo msim.
Amesema kata tatu za Ugalla,Mtapenda na Nsimbo za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kati ya kata 12 za Halmashauri hiyo ndizo ambazo zimechaguliwa kuanzisha kilimo cha zao hilo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Lilian Matinga amesema wanafanya utafiti kuhusu zao la korosho ambapo mpaka sasa wamesia mbegu za korosho kilogramu kumi kwa ajili ya kuanza kulima zao hilo kwa mwaka huu.
Mwezi uliopita,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa kumi akiwemo mkuu wa Mkoa wa Katavi kuanzisha kilimo cha zao la pamba kwa ajili ya kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA