MANISPAA YA MPANDA WAIBUKA NA MASTA PLAN YA MPANGO MJI,MKUU WA MKOA WA KATAVI ATOA NENO-Oktoba 6,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Jengo la Ofisi za Manispaa ya Mpanda na Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amewataka wananchi mkoani Katavi,kuacha tabia ya kuzuia miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Muhuga ametoa kauli  hiyo leo katika kikao cha wadau wa Mpango Kabambe (Master Plan) kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda ambapo amesema lengo kubwa la Mkoa ni kuwa na mji uliopangika vizuri lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa wakikwamisha.
Aidha amewataka  viongozi wa mitaa pamoja na Kata kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wa Mpango huo ili wafanye kazi vizuri sambamba na kuwashirikisha wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mipango Miji Mshauri kutoka City Plan Consultants LTD ya Dar es salaam Bw.Iddy Mwerangi amesema,Mpango kabambe una majukumu mengi ikiwemo kupitia mipango ya maendeleo iliyopo na kufanya utekelezaji wake pamoja na  Kutoa mapendekezo yanayokidhi matakwa ya kisheria.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bi.Enelia Lutungulu amewasistiza viongozi kuwahamasisha wananchi ili mpango uende vizuri.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni miongoni mwa halmashauri hapa nchini zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na benki ya dunia ambapo pamoja na Miradi mingine Halmashauri ya manispaa ya Mpanda inaandaa mpango kabambe maarufu kama Master Plan utakaoongoza matumizi ya ardhi ya manispaa ya Mpanda kwa kipindi  miaka 20 ijayo.
Mpango mchakato huo uliokuwa umeanza tangu mwaka 2010, haukufika mwisho kwa sababu ya ongezeko la mahitaji ikiwa ni pamoja na ongezeko la ukubwa wa eneo la kiutawala manispaa ya Mpanda hivyo kupelekea kuanza upya Mchakao huo kwa kuwa taarifa za awali za msingi zilipitwa na muda wake.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA