DC MPANDA-HAKUNA PEMBEJEO ZA RUZUKU-Oktoba 6,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Wa kwanza kulia ni DC llilian Matinga(asiyekuwa na wigi)
MKUU wa wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga, amesema wakulima wilayani Mpanda wasitegemee mbolea za pembejeo za ruzuku pekee kwa kuwa mpaka sasa hakuna mwongozo wowote kuhusu pembejeo hizo kuwepo.

Matinga amebainisha hatua hiyo wakati akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake kuhusu dalili za kucheleweshwa kwa pembejeo hizo wakati ndiyo msimu wa kilimo ambapo amewataka waendelee kununua katika maduka yanayouza mbolea.
Wakulima wameanza kusikika wakilalamikia serikali kuchelewesha kuleta mbolea kwa ajili ya kuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija.
Kuanzia mwaka 2015,Wakuu wa wilaya na wakuu wa Mikoa hapa nchini waliagizwa na serikali kuu kusimamia usambazaji wa mbolea tofauti na mfumo uliokuwepo wa mawakala kufanya kazi hiyo.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA