GODBLESS LEMA : KAMA SERIKALI YA MAGUFULI HAIJUI NANI ANAEFANYA MATUKIO YA MAUAJI, BASI NAE HAYUKO SALAMA-Oktoba 6,2017

Godbless Lema akizungumza(mwenye shati (jeupe) na waandishi wa habari
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehoji maswali mbalimbali kwa  Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP),Simon Sirro kuhusu mambo yanayoendelea kwenye upelelezi wa Ben Saanane,Tundu Lissu na aliyemtishia Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye.

Akizungumza katika mkutano na wandishi wa habari Waziri kivuli wa mambo ya ndani na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema,amewahoji viongozi hao,namna amabavyo wamekuwa wakishughulikia masuala yanayohatarisha usalama wa nchi.
Katika mkutano huo mh Lema amesema swala la usalama  wa nchi na maisha ya kila mtanzania yanamuhusu kila mmoja hapa nchini hususani waandishi wa habari.
’Tuna IGP anaefikiri kuwa kamanda mkakamavu ni kubeba siraha,na mimi nataka nimwambie siro huwezi kuprove kwamba wewe ni kamanda kwa sababu umezungukwa na watu wenye bunduki,utaprove kwamba wewe ni kamanda kama unaweza ukacary on the truth, “amesema mh, lema”
Mh,lema amesema kuwa wananchi wameendelea kupoteza matumaini na jeshi la polisi kutokana hilo kutokuchukua hatua haraka katika baadhi ya matukio amabyo yameendelea kutokea hapa nchini.
Aidha amesema yeye yupo kwenye tageti ya kuuwawa kwa kuwa kilichotokea kwa mh lisu ni mwendelezo wa mambo mengi yanaoweza kutokea kwa viongozi wao.
Katika hatua nyingine amesema  ofisi ya IGP,idara ya usalama wa taifa,pamoja na waziri wa mambo ya ndani wao kama hawajui watuhumiwa na kusema ni watu wasiojulikana,kama waziri anasema kuna watu wasiojulika basi waziri hatakiwi kujulikana kama yupo ofsini.
Hata hivyo mh Lema amesema rais magufuli ajue kuwa wao wanamwili,wanadamu na pia wanandugu,na kama serikali ya magufuli haijui nani anaefanya matukio hayo basi yeye mwenye hayuko salama,na kama yeye mwenye hayupo salama kwa nini ameyanamazia?.huku akinukuu maneno ya biblia, uwa kama ilivyoandikwa yanayofanyika dalini yatasitirika hadharani,ambapo amesema hivi karibuni mambo yote yatasitirika hadharani. 

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA