UNGUJA ZANZIBAR:KILIMO CHA ASILI NI KIVUTIO NJE YA NCHI-Oktoba 6,2017

IMEELEZWA kuwa kilimo cha asili kisichotumia kemikali ni kivutio kwa idadi kubwa nchi za nje kuthamini ubora wa bidhaa za Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa bodi kutoka Jumuia ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima Ahmed Saleh Mbarouk wakati akizungumza na Maisha  fm radio.
Amesema kutokana na ubora wa kilimo cha mboga mboga kinacholimwa Zanzibar ni vyema wakulima kuendeleza kilimo hicho ili kuongeza kasi ya biashara za nje ya nchi.
Mjumbe huyo amefahamisha kuwa suala la kusarifu vyakula kutaweza kupunguza wimbi la matunda kuharibika wakati wa mavuno sambamba na kusubiri soko na kuongeza pato la wakulima.
Aidha ameziomba taasisi kuwa na ubunifu wa kuwawezesha wakulima kuwapatia nyezo za kusarifia mazao ili kumuwezesha mkulima kuwa na kilimo chenye tija.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA