SHIRIKA LA WATERLEED WAMETOA MSAADA WA GARI 1 NA PIKIPIKI 26 KATIKA MKOA WA KATAVI

Na.Issack Gerald-Katavi
Shirika la Waterleeds  Program  Tanzani  WRP-T limetoa msaada wa  gari moja kwa  Manispaa ya  Mpanda na pikipiki 26 kwa Halmashauri za mkoa wa  Katavi zenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 268.

Msaada huo uliokabidhiwa jana  na mkuu wa mkoa wa Katavi Meja  Gegerali Mstaafu  Raphael Muhuga kwa  halmashauuri zote  tano za mkoa wa Katavi  ni kwa ajili ya  shughuli za  mradi wa kudhibiti  Ukimwi mkoani Katavi.
Akitoa taarifa ya  msaada huo afisa mradi huo WRP-T mkoani Katavi  Dkt Baraka Mgiriwa amesema  msaada huo wa  gari  moja na pikipiki 26 umegharimu  kiasi cha shilingi milioni 268
Alisema  katika  msaada huo  Manispaa ya Mpanda wamepata   gari moja  aina ya  Picup  Land  Cruiser lenye  thamani ya shilingi milioni 168,987.707 pikipiki 4 aina ya  Honda, Halmashauri ya Mpanda imepata pikipiki 5, halmashauri ya Mlele  pikipiki 5, halmashauri ya Nsimbo pikipiki 6, halmashauri ya Mpimbwe pikipiki 5 na   ofisi ya  Mganga Mkuu wa  Mkoa  ilipata pikipiki  moja zote zikiwa  na  thamani ya shilingi milioni 98,800,000.
Kwaupande wake mganga mkuu  wa mkoa huo  wa Katavi  Dkt Yahaya  Huseein alisema baada ya halmashauri hizo kukabidhiwa misaada hiyo  wana matarajio makubwa ya kutoa  huduma mbalimbali  katika  maeneo ya halmashauri hizo.
Alizitaja baadhi ya huduma  hizo kuwa ni kuimarika  kwa  shughuli  za usafirishaji wa  sampuli za damu kavu za watoto waliozaliwa na wakina mama wenye  maambukizi ya VVU  kwa ajiri  ya kupimwa  hali ya maambukizi ya watoto wao .
Pia alisema kazi nyingine ni kupunguza uharibifu wa sampuli  za  damu  kwa watoto  waliozaliwa  na mama  wenye VVU   pamoja  na zile za kupima  wingi  wa kiwango  cha vvu  katika  damu  kwa WAVIU  wote  kwani kabla ya msaada huo walikua wakichelewa  kusafirishwa vipimo kwenda katika  maabara.
Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi Raphael  Muhuga alisema msaada huo utasaidia kuboresha  utendaji kazi kwa wagonjwa  kupatiwa huduma kwa wakati tofauti  na ilivyokua  hapo  awali ambapo amezitaka halmashauri  zote za mkoa wa Katavi zione  umuhimu wa   kuvitunza  vitendea kazi hivyo na wavitumie kwa makusudi yaliokusudiwa na si tofauti.

Kwa upande wake mkurugenzi wa  Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe  Erasto  Kiwale  amesema    kutoka na jografia ya halmashauri  yake, pikikpiki   hizo  zitawasaidia  watumishi wa  afya kwenda kutoa huduma kwenye maeneo ambayo  hayafikiki kwa  gari kwa urahisi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA