AJALI YA MOTO IMEUA WATU 4 USIKU WA KUAMKIA LEO

Watu wanne wamepoteza maisha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha fumba wilaya ya Magharibi B Unguja kutokana na nyumba kuteketea kwa moto mnamo majira ya saa sita na nusu usiku.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Hassan Nassir Ali amewataja waliofariki ni Bahati Ali Ameir (40), Sinawema Abdalla Ali (10), Hashim Abdalla (6) na Latifa Mohammed Ali (8).

Kamanda wa polisi amesema tukio hilo linaaminika limesababishwa  na hitilafu ya umeme na kuwataka wananchi kuwa waangalifu katika matumizi yao ya umeme.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA