RAIS MGABE AMETEULIWA NA UN KUWA BALOZI MWEMA WA AFYA

Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika .
Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo,Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O.Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus,alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.
Lakini wakosoaji wamesema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe,huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .

Dr.Tedros ni raia wa Ethiopia ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA