AJALI YA NDEGE CHINI KENYA

Ndege moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.

Afisa mkuu wa Polisi mjini Nakuru Joshua Omukata amethibitisha kisa hicho akisema walikuwa wakisubiri boti kufanya operesheni ya kuwanusuru waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.
Ripoti zinasema kuwa kulikuwa na watu watano katika ndege hiyo ambapo Seneta wa Nakuru Susan Kihika amesema watatu kati ya wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa wanachama wa kitengo chake cha mawasiliano.
Ndege hiyo iliondoka katika hoteli ya Jarika County Lodge na taarifa zinasema ilikuwa ikipaa chini chini kabla ya kuanguka ambapo Ndge hiyo ilitarajiwa kusafrisha waandishi wa habari katika mkutano wa kampeni .
Waokoaji walikuwa bado hawajaanza operesheni saa nne baada ya ndege hiyo kuanguka katika ziwa hilo kwa ukosefu wa boti.

Waokoaji walilazimika kusubiri boti kusafirishwa kutoka Ziwa Naivasha huku Mkurugenzi wa Idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga Pius Masai akisema ndege ya polisi imetumwa katika eneo hilo kusaidia katika uokoaji.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA