BANGI,NYARA ZA SERIKALI ZAWAPELEKA WATU 40 MIKONONI MWA POLISI



JESHI la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 46 wa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na nyara za serikali zenye dhamani ya zaidi ya shilingi million 20.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni iliyofanywa kuanzia octoba 4 hadi 12 mwaka huu ikihusisha taasisi mbalimbali zikiwemo shirika la umeme nchini (TANESCO), Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA),Uhamiaji,Maliasili na Polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto,amesema katika oparesheni hiyo zimekamatwa nyara za serikali ambazo ni ngozi mbili za mnyama aina ya chui zenye thamani ya shilingi milioni 15,750,000,nyama ya mnyamapori aina ya tandara kilogram tatu zenye thamani ya sh. 5,700,000.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo limekamata pikipiki tano za wizi pamoja na pikipiki zaidi ya 500 zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.
Wakati huo huo amesema kuhusu mazao ya misitu walikamata mbao 200,mkaa pamoja na makosa ya kuharibu misitu na kufanya shughuli za kuchoma mkaa katika maeneo ya hifadhi.
Hata ameonya tabia ya baadhi ya wazazi kuingia mkataba na dereva wa bodaboda kupakia watoto kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani ambapo kamanda Muroto amewataka waalimu kutowapokea wanafunzi wanaotumia usafiri huo.
Oparesheni hiyo pia ilishirikisha mataifa wanachama wa shirikisho la polisi Afrika mashariki na kusini mwa afrika chini ya shirikisho la polisi Interpol ,lengo likiwa ni kukabili hali ya uharifu wa makosa mtambuka yanayovuka mipaka ya nchi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA